Monday, May 13, 2013

29th ALAT AGM in Pictures

The 29th ALAT AGM and Expo was held at Sundown Carnival in Arusha. An ideal venue for Local Government leaders and partners alike to meet and address key issues at an absolute serene environment surrounded by vast landscapes of green.
















The 29th AGM kept much in line with adopted approach by the current ALAT leadership of PPP. Giving opportunities for businesses and Government Institutions to participate by either sponsoring or exhibition of relates products and services.
The AGM was officially opened by Hon. Prime Minister Mizengo Pinda on the 9th May,2013. There after followed by a meet and greet cocktail evening.
On the 10th - 11th May,2013 were dedicated to ALAT related issues along with partner presentations.






See you in Tanga for The 30th AGM 2014
Event Management by Vision Investments www.vision.co.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari (Press Conference) 29th ALAT AGM 2013


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO MKUU WA 29 WA ALAT - ARUSHA
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 29 tarehe 9 – 11 Mei 2013. Mkutano huo utafanyika katika  Ukumbi wa Sundown Canivore, jijini Arusha.
Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa 29 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni “Mafanikio ya miaka 51 ya Uhuru yatumike katika kuimarisha uchumi katika jamii.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni: Wenyeviti na Mameya 161 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 161 wa Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa. Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta Binafsi.  Inatarajiwa kwamba Mkutano huu utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (500).

Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 161 zinazounganishwa na chombo hiki.
Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa 29 wa ALAT ni Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb) waziri Mkuu wa Jamhuri ya
ALAT imedhamiria kutumia Mkutano wake Mkuu wa mwaka huu kuendelea kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano baina ya sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP). AIdha mkutano huu utatumika kuhamasisha ushiriki wa Serikali za mitaa kwenye mchakato wa uandaaji wa katiba mpya.
Mkutano huu ambao mwenyeji wake ni jiji la Arusha, utatanguliwa na Jukwaa la Ubadilishanaji Uzoefu juu ya Ubia Baina ya Serikali na Sekta Binafsi katika kutoa huduma kwa jamii na hasa katika kuzitumia Serikali za Mitaa. Ifahamike kuwa Serikali za mitaa zina  fursa ‘potential’ kubwa  na  nyingi za kutekeleza ubia kwa kufanya mashirikiano yenye manufaa na sekta binafsi. ALAT imeona kuna haja na umuhimu wa kuandaa jukwaa hili kwa wanachama wake kwani ni lenye manufaa makubwa ya kuwakutanisha viongozi na watendaji wa Halmashauri zote nchini kuweza  kujifunza na kufahamu kwa mapana zaidi dhana ya ubia na uhalisia uliopo katika utekelezaji wake (Practicalities).
Aidha hii ni fursa ya pekee kwa sekta binafsi, taasisi za Serikali na mashirika ya Umma kuweza kushiriki pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa kujadili jambo lenye manufaa kwa pande zote. Jukwaa la ubadilishanaji uzoefu litakaloongozwa na wataalamu waliobobea katika nyanja za kuimarisha uchumi katika ngazi ya Jamii , Local Economic Development. Mada zitakazojadiliwa ni pamoja na maana halisi ya dhana ya ukuzaji uchumi katika jamii umuhimu wa  taasisi za kifedha  katika kusaidia uendelezaji uchumi katika Jamii pamoja na  mada ya fursa zilizopo katika Halmashauri za  mijini na zile za wilaya katika ukusanyaji wa rasilimali (fedha).
Viongozi wa Serikali wamealikwa kutengeneza jopo la wasemaji. Miongoni mwa wanaotarajiwa ni Mhe. Stephen Wassira – Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Uhusiano, Mhe. Sospeter Muhongo (mb) Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (Mb) Waziri wa Maji Mhe. Hawa Abdur Rahman Ghasia (Mb) Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Gaudensia Kabaka (mb) Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Emanuel Nchimbi (mb) Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.  Profesa Ana Tibaijuka (mb) Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (mb) Waziri wa Maliasili na Utalii. Wengine ni Waziri wa Afya Dr Hussein Mwinyi (mb), Mhe. Dr John Pombe Magufuli (mb) – Waziri wa Ujenzi, Mhe. Mary Nagu (mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji na Mhe.  Makongoro Mahanga (mb) Naibu Waziri Kazi na Ajira. Waalikwa wengine ni pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Bwana Hari Kitilya, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Huduma za Manunuzi Dr. Ramadhani Mlinga pamoja na Mwakilishi wa Benki ya Dunia. Jumuiya imemwalika Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Fedha za Serikali (CAG) Ndugu Ludovick Utouh ambaye atawasilisha Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Fedha za Serikali za Mitaa.
Maandalizi ya Mkutano yamekamilika na ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wabia na wadhamini walioweza kujitokeza kutuunga mkono katika Mkutano huu; NMB ambaye ni mdhamini mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), TASAF, na PSPF. Wengine ni PPF, Mamlaka ya viwanja vya ndege, Tanzania Standard Newspaper na GF trucks.
________________________________________
Dr. Didas  Massaburi – Mwenyekiti ALAT (T)
na Mstahiki Meya wa Jiji  la Dar es Salaam.     Leo Jumatano, tarehe 8 Mei 2013.

29TH ALAT AGM