TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO
MKUU WA 29 WA ALAT - ARUSHA
Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 29 tarehe 9 – 11 Mei 2013.
Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Sundown
Canivore, jijini Arusha.
Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa 29
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni “Mafanikio ya miaka 51 ya Uhuru
yatumike katika kuimarisha uchumi katika jamii”.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa
Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni: Wenyeviti na Mameya
161 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 161 wa
Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na
Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika
Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika
ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau
wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa. Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi
zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta
Binafsi. Inatarajiwa kwamba Mkutano huu
utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (500).
Jumuiya ya Tawala za Mitaa
Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji, Manispaa
na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 161 zinazounganishwa na
chombo hiki.
Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa
29 wa ALAT ni Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb) waziri
Mkuu wa Jamhuri ya
ALAT imedhamiria kutumia Mkutano
wake Mkuu wa mwaka huu kuendelea kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano
baina ya sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP). AIdha mkutano huu utatumika kuhamasisha
ushiriki wa Serikali za mitaa kwenye mchakato wa uandaaji wa katiba mpya.
Mkutano huu ambao mwenyeji wake
ni jiji la Arusha, utatanguliwa na Jukwaa la Ubadilishanaji Uzoefu juu ya Ubia Baina
ya Serikali na Sekta Binafsi katika kutoa huduma kwa jamii na hasa katika kuzitumia
Serikali za Mitaa. Ifahamike kuwa Serikali za mitaa zina fursa ‘potential’ kubwa na
nyingi za kutekeleza ubia kwa kufanya mashirikiano yenye manufaa na
sekta binafsi. ALAT imeona kuna haja na umuhimu wa kuandaa jukwaa hili kwa wanachama
wake kwani ni lenye manufaa makubwa ya kuwakutanisha viongozi na watendaji wa
Halmashauri zote nchini kuweza kujifunza
na kufahamu kwa mapana zaidi dhana ya ubia na uhalisia uliopo katika
utekelezaji wake (Practicalities).
Aidha hii ni fursa ya pekee kwa
sekta binafsi, taasisi za Serikali na mashirika ya Umma kuweza kushiriki pamoja
na viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa kujadili jambo lenye manufaa kwa
pande zote. Jukwaa la ubadilishanaji uzoefu litakaloongozwa na wataalamu waliobobea
katika nyanja za kuimarisha uchumi katika ngazi ya Jamii , Local Economic
Development. Mada zitakazojadiliwa ni pamoja na maana halisi ya dhana ya
ukuzaji uchumi katika jamii umuhimu wa taasisi za kifedha katika kusaidia uendelezaji uchumi katika
Jamii pamoja na mada ya fursa zilizopo
katika Halmashauri za mijini na zile za
wilaya katika ukusanyaji wa rasilimali (fedha).
Viongozi wa Serikali wamealikwa
kutengeneza jopo la wasemaji. Miongoni mwa wanaotarajiwa ni Mhe. Stephen
Wassira – Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Uhusiano, Mhe. Sospeter Muhongo (mb)
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (Mb) Waziri wa Maji Mhe.
Hawa Abdur Rahman Ghasia (Mb) Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Gaudensia Kabaka (mb) Waziri
wa Kazi na Ajira, Mhe. Emanuel Nchimbi (mb) Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Profesa Ana Tibaijuka (mb) Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (mb) Waziri wa
Maliasili na Utalii. Wengine ni Waziri wa Afya Dr Hussein Mwinyi (mb), Mhe. Dr
John Pombe Magufuli (mb) – Waziri wa Ujenzi, Mhe. Mary Nagu (mb) Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji na Mhe. Makongoro Mahanga (mb) Naibu Waziri Kazi na
Ajira. Waalikwa wengine ni pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini
Bwana Hari Kitilya, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Huduma za Manunuzi Dr.
Ramadhani Mlinga pamoja na Mwakilishi wa Benki ya Dunia. Jumuiya imemwalika
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Fedha za Serikali (CAG) Ndugu Ludovick
Utouh ambaye atawasilisha Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Fedha za Serikali za
Mitaa.
Maandalizi ya Mkutano yamekamilika
na ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wabia na wadhamini walioweza kujitokeza
kutuunga mkono katika Mkutano huu; NMB ambaye ni mdhamini mkuu, Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), TASAF, na PSPF. Wengine
ni PPF, Mamlaka ya viwanja vya ndege, Tanzania Standard Newspaper na
GF trucks.
________________________________________
Dr. Didas Massaburi –
Mwenyekiti ALAT (T)
na Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Leo Jumatano, tarehe 8 Mei 2013.
No comments:
Post a Comment