Thursday, May 1, 2014

30TH NMB ALAT AGM & EXPO in Tanga


JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO MKUU WA 30 WA ALAT - TANGA
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 30 tarehe 7 – 10 Mei 2014. Mkutano huo unaodhaminiwa na benki ya NMB utafanyika katika  Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivara Jijini Tanga. Kauli Mbiu ya Mkutano huu ambao pia utaanzisha mchakato wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 30 tangu kuanzishwa upya kwa mfumo wa Serikali za Mitaa hapa nchini na pia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) mwaka 1984 ni “Miaka 30 ya Serikali za Mitaa na


ALAT: Katiba Bila Sura ya Serikali za Mitaa ni Kudhoofisha  Demokrasia ya Wananchi “.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni: Wenyeviti na Mameya 168 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 168 wa Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa. Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta Binafsi.  Inatarajiwa kwamba Mkutano huu utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (500).
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 168 zinazounganishwa na chombo hiki.
(C) Hon. Dr. Didas Massaburi addressing journalists not in picture flanked (r) by Mr. Habraham Shamumoyo Exec. Secretary of ALAT
Mkutano Mkuu wa 30 wa ALAT ni Mkutano wa aina ya pekee kwa sababu tatu zifuatazo;- (i) Jumuiya inafikisha miaka 30 tangu kuundwa kwake, (ii) ni miaka 30 tangu nchi yetu irudishe tena mfumo wa serikali za mitaa na hivyo tumejifunza na kupata uzoefu wa kutosha katika ugatuaji wa madaraka na (iii) ni mwaka ambao nchi yetu inapitia hatua muhimu ya kuunda  Katiba yake mpya.
Kutokana na maombi kutoka kwa wadau mbalimbali imedhamiriwa kwamba Mkutano Mkuu wa 30 ambao mwenyeji waki ni Jiji la Tanga,  utatoa fursa ya kipekee ya kuendelea kuwa jukwaa la  kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano baina ya sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP). Aidha katika kulitekeleza hilo Mkutano wa 30 umeongeza siku zake kuwa nne ili kutoa fursa ya kutosha kwa wanachama na wadau mbalimbali kupeana uzoefu wa mambo mbalimbali yanayaohusu sekta ya Serikali za Mitaa, sekta ya fedha na biashara, sekta binafsi na jamii kwa ujumla. Aidha muundo wa Mkutano mkuu umepanuliwa zaidi katika kutoa fursa ya kufanya sambamba mikutano mingine midogo (parallel Sessions) ili kuwawezesha washiriki wa Mkutano waweze kuketi katika makundi yenye kutoa huduma za pamoja katika Serikali za Mitaa na kujadili kwa ufasaha zaidi mambo yanyowasibu katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku pamoja na kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo.
Aidha hii ni fursa nyingine kubwa na ya pekee kwa sekta binafsi, taasisi za Serikali na mashirika ya Umma kuweza kushiriki pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa kujadili jambo lenye manufaa kwa pande zote. Mikutano pacha itakayoongozwa na wataalamu waliobobea katika nyanja za kuimarisha uchumi katika ngazi ya Jamii (Local Economic Development), utoaji wa huduma bora kwa jamii na utunzaji wa mazingira katika miji.
NMB Bank handing over a dummy sponsorship cheque of Tsh150 million
Tunaishukuru kwa namna ya Pekee Benki  ya NMB kwa kuwa ni mdau (patner) katika mkutano huu. Benki ya NMB ni kielelezo tosha cha uhusiano, ushirikiano na utoaji wa huduma kwa serikali za mitaa. Tunazialika taasisi nyingine za Serikali, binafsi na mashirika ya hiari kuja kushiriki nasi katika Mkutano huu muhimu kupitia ufadhili kwani bado fursa zipo.
Maandalizi ya awali ya Mkutano huu yameshafanywa ikiwa ni pamoja na kuwaalika wanachama, Serikali, Mashirika yasiyo ya kiserikali, Wafadhili na wadau mbalimbali. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mhe Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

-MWISHO-

________________________________________
Dr. Didas Massaburi – Mwenyekiti ALAT (T) na Mstahiki Meya wa Jiji  la Dar es Salaam.  

Tuesday, February 4, 2014

ALAT to back pro-devolution presidential candidate

Arusha. The  Association of Local Authorities of Tanzania (ALAT) declared yesterday that it would rally behind and support any presidential candidate who will show readiness to improve local democratic governance by implementing the policy of decentralization by devolution.
Tanzania adopted decentralisation legislation in the late 1990s, which aims to devolve significant powers to locally elected urban and rural councils to manage manpower, revenue generation, planning and budgeting.
ALAT chairman Didas Masaburi gave the position in Arusha yesterday when closing a four-day training  programme on capacity building for local experts and councillors from various district councils across the country.
“Some people are moving here and there in search of the presidency;  ALAT openly declares that we will support a candidate who will be ready to implement the policy of decentralization by devolution that gives wananchi more power to manage their affairs,” said Mr Masaburi, who   is also the mayor of Dar es Salaam.
He said the policy has been in existence for  a long time but has never been implemented fully, the trend he blamed for retarding the development  of people in villages despite government efforts to build more roads  to connect all regions and districts.  

ALAT wants observer status in EAC

The Association of Local Authorities of Tanzania (ALAT) wants to be granted an observer status in the Arusha-based, East African Community (EAC). Speaking in Arusha, the Chairperson of ALAT Dr Didas Masaburi, pointed out that if the current EAC wishes to be people-centred as it claims, then it cannot avoid including local area authorities from the community’s five member states.

Dr Masaburi, who was accompanied by the association’s Secretary, Mr Habram Shamumoyo, was speaking at the climax of the local authority’s constitutional council held in the city.
The assembly had made various recommendations for the 2013 draft constitution, including a need to make the immigration department part of the official security organs.
“Other than just having the army and the police there is need to have the immigration department recognized as an important organ in the official security sector,” stated the ALAT chairman.
The ALAT meeting on constitution reforms made a stab on the proposed three governments system where some of the people who contributed called for the re-establishment of the mainland (Tanganyika) government to operate in-sync with the Zanzibar Government and then form the overall federal Tanzanian government.
“Three governments will be expensive and cumbersome to run and why should we have a federal government at the threshold of forming the East African Federation?” asked Dr Masaburi.
By MARC NKWAME, Tanzania Daily News

Monday, May 13, 2013

29th ALAT AGM in Pictures

The 29th ALAT AGM and Expo was held at Sundown Carnival in Arusha. An ideal venue for Local Government leaders and partners alike to meet and address key issues at an absolute serene environment surrounded by vast landscapes of green.
















The 29th AGM kept much in line with adopted approach by the current ALAT leadership of PPP. Giving opportunities for businesses and Government Institutions to participate by either sponsoring or exhibition of relates products and services.
The AGM was officially opened by Hon. Prime Minister Mizengo Pinda on the 9th May,2013. There after followed by a meet and greet cocktail evening.
On the 10th - 11th May,2013 were dedicated to ALAT related issues along with partner presentations.






See you in Tanga for The 30th AGM 2014
Event Management by Vision Investments www.vision.co.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari (Press Conference) 29th ALAT AGM 2013


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO MKUU WA 29 WA ALAT - ARUSHA
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 29 tarehe 9 – 11 Mei 2013. Mkutano huo utafanyika katika  Ukumbi wa Sundown Canivore, jijini Arusha.
Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa 29 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni “Mafanikio ya miaka 51 ya Uhuru yatumike katika kuimarisha uchumi katika jamii.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni: Wenyeviti na Mameya 161 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 161 wa Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa. Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta Binafsi.  Inatarajiwa kwamba Mkutano huu utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (500).

Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 161 zinazounganishwa na chombo hiki.
Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa 29 wa ALAT ni Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb) waziri Mkuu wa Jamhuri ya
ALAT imedhamiria kutumia Mkutano wake Mkuu wa mwaka huu kuendelea kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano baina ya sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP). AIdha mkutano huu utatumika kuhamasisha ushiriki wa Serikali za mitaa kwenye mchakato wa uandaaji wa katiba mpya.
Mkutano huu ambao mwenyeji wake ni jiji la Arusha, utatanguliwa na Jukwaa la Ubadilishanaji Uzoefu juu ya Ubia Baina ya Serikali na Sekta Binafsi katika kutoa huduma kwa jamii na hasa katika kuzitumia Serikali za Mitaa. Ifahamike kuwa Serikali za mitaa zina  fursa ‘potential’ kubwa  na  nyingi za kutekeleza ubia kwa kufanya mashirikiano yenye manufaa na sekta binafsi. ALAT imeona kuna haja na umuhimu wa kuandaa jukwaa hili kwa wanachama wake kwani ni lenye manufaa makubwa ya kuwakutanisha viongozi na watendaji wa Halmashauri zote nchini kuweza  kujifunza na kufahamu kwa mapana zaidi dhana ya ubia na uhalisia uliopo katika utekelezaji wake (Practicalities).
Aidha hii ni fursa ya pekee kwa sekta binafsi, taasisi za Serikali na mashirika ya Umma kuweza kushiriki pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa kujadili jambo lenye manufaa kwa pande zote. Jukwaa la ubadilishanaji uzoefu litakaloongozwa na wataalamu waliobobea katika nyanja za kuimarisha uchumi katika ngazi ya Jamii , Local Economic Development. Mada zitakazojadiliwa ni pamoja na maana halisi ya dhana ya ukuzaji uchumi katika jamii umuhimu wa  taasisi za kifedha  katika kusaidia uendelezaji uchumi katika Jamii pamoja na  mada ya fursa zilizopo katika Halmashauri za  mijini na zile za wilaya katika ukusanyaji wa rasilimali (fedha).
Viongozi wa Serikali wamealikwa kutengeneza jopo la wasemaji. Miongoni mwa wanaotarajiwa ni Mhe. Stephen Wassira – Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Uhusiano, Mhe. Sospeter Muhongo (mb) Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (Mb) Waziri wa Maji Mhe. Hawa Abdur Rahman Ghasia (Mb) Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Gaudensia Kabaka (mb) Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Emanuel Nchimbi (mb) Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.  Profesa Ana Tibaijuka (mb) Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (mb) Waziri wa Maliasili na Utalii. Wengine ni Waziri wa Afya Dr Hussein Mwinyi (mb), Mhe. Dr John Pombe Magufuli (mb) – Waziri wa Ujenzi, Mhe. Mary Nagu (mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji na Mhe.  Makongoro Mahanga (mb) Naibu Waziri Kazi na Ajira. Waalikwa wengine ni pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Bwana Hari Kitilya, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Huduma za Manunuzi Dr. Ramadhani Mlinga pamoja na Mwakilishi wa Benki ya Dunia. Jumuiya imemwalika Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Fedha za Serikali (CAG) Ndugu Ludovick Utouh ambaye atawasilisha Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Fedha za Serikali za Mitaa.
Maandalizi ya Mkutano yamekamilika na ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wabia na wadhamini walioweza kujitokeza kutuunga mkono katika Mkutano huu; NMB ambaye ni mdhamini mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), TASAF, na PSPF. Wengine ni PPF, Mamlaka ya viwanja vya ndege, Tanzania Standard Newspaper na GF trucks.
________________________________________
Dr. Didas  Massaburi – Mwenyekiti ALAT (T)
na Mstahiki Meya wa Jiji  la Dar es Salaam.     Leo Jumatano, tarehe 8 Mei 2013.

29TH ALAT AGM