Tuesday, February 4, 2014

ALAT to back pro-devolution presidential candidate

Arusha. The  Association of Local Authorities of Tanzania (ALAT) declared yesterday that it would rally behind and support any presidential candidate who will show readiness to improve local democratic governance by implementing the policy of decentralization by devolution.
Tanzania adopted decentralisation legislation in the late 1990s, which aims to devolve significant powers to locally elected urban and rural councils to manage manpower, revenue generation, planning and budgeting.
ALAT chairman Didas Masaburi gave the position in Arusha yesterday when closing a four-day training  programme on capacity building for local experts and councillors from various district councils across the country.
“Some people are moving here and there in search of the presidency;  ALAT openly declares that we will support a candidate who will be ready to implement the policy of decentralization by devolution that gives wananchi more power to manage their affairs,” said Mr Masaburi, who   is also the mayor of Dar es Salaam.
He said the policy has been in existence for  a long time but has never been implemented fully, the trend he blamed for retarding the development  of people in villages despite government efforts to build more roads  to connect all regions and districts.  

ALAT wants observer status in EAC

The Association of Local Authorities of Tanzania (ALAT) wants to be granted an observer status in the Arusha-based, East African Community (EAC). Speaking in Arusha, the Chairperson of ALAT Dr Didas Masaburi, pointed out that if the current EAC wishes to be people-centred as it claims, then it cannot avoid including local area authorities from the community’s five member states.

Dr Masaburi, who was accompanied by the association’s Secretary, Mr Habram Shamumoyo, was speaking at the climax of the local authority’s constitutional council held in the city.
The assembly had made various recommendations for the 2013 draft constitution, including a need to make the immigration department part of the official security organs.
“Other than just having the army and the police there is need to have the immigration department recognized as an important organ in the official security sector,” stated the ALAT chairman.
The ALAT meeting on constitution reforms made a stab on the proposed three governments system where some of the people who contributed called for the re-establishment of the mainland (Tanganyika) government to operate in-sync with the Zanzibar Government and then form the overall federal Tanzanian government.
“Three governments will be expensive and cumbersome to run and why should we have a federal government at the threshold of forming the East African Federation?” asked Dr Masaburi.
By MARC NKWAME, Tanzania Daily News

Monday, May 13, 2013

29th ALAT AGM in Pictures

The 29th ALAT AGM and Expo was held at Sundown Carnival in Arusha. An ideal venue for Local Government leaders and partners alike to meet and address key issues at an absolute serene environment surrounded by vast landscapes of green.
















The 29th AGM kept much in line with adopted approach by the current ALAT leadership of PPP. Giving opportunities for businesses and Government Institutions to participate by either sponsoring or exhibition of relates products and services.
The AGM was officially opened by Hon. Prime Minister Mizengo Pinda on the 9th May,2013. There after followed by a meet and greet cocktail evening.
On the 10th - 11th May,2013 were dedicated to ALAT related issues along with partner presentations.






See you in Tanga for The 30th AGM 2014
Event Management by Vision Investments www.vision.co.tz

Taarifa kwa Vyombo vya Habari (Press Conference) 29th ALAT AGM 2013


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO MKUU WA 29 WA ALAT - ARUSHA
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 29 tarehe 9 – 11 Mei 2013. Mkutano huo utafanyika katika  Ukumbi wa Sundown Canivore, jijini Arusha.
Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa 29 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni “Mafanikio ya miaka 51 ya Uhuru yatumike katika kuimarisha uchumi katika jamii”.
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni: Wenyeviti na Mameya 161 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 161 wa Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa. Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta Binafsi.  Inatarajiwa kwamba Mkutano huu utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (500).

Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 161 zinazounganishwa na chombo hiki.
Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa 29 wa ALAT ni Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb) waziri Mkuu wa Jamhuri ya
ALAT imedhamiria kutumia Mkutano wake Mkuu wa mwaka huu kuendelea kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano baina ya sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP). AIdha mkutano huu utatumika kuhamasisha ushiriki wa Serikali za mitaa kwenye mchakato wa uandaaji wa katiba mpya.
Mkutano huu ambao mwenyeji wake ni jiji la Arusha, utatanguliwa na Jukwaa la Ubadilishanaji Uzoefu juu ya Ubia Baina ya Serikali na Sekta Binafsi katika kutoa huduma kwa jamii na hasa katika kuzitumia Serikali za Mitaa. Ifahamike kuwa Serikali za mitaa zina  fursa ‘potential’ kubwa  na  nyingi za kutekeleza ubia kwa kufanya mashirikiano yenye manufaa na sekta binafsi. ALAT imeona kuna haja na umuhimu wa kuandaa jukwaa hili kwa wanachama wake kwani ni lenye manufaa makubwa ya kuwakutanisha viongozi na watendaji wa Halmashauri zote nchini kuweza  kujifunza na kufahamu kwa mapana zaidi dhana ya ubia na uhalisia uliopo katika utekelezaji wake (Practicalities).
Aidha hii ni fursa ya pekee kwa sekta binafsi, taasisi za Serikali na mashirika ya Umma kuweza kushiriki pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa kujadili jambo lenye manufaa kwa pande zote. Jukwaa la ubadilishanaji uzoefu litakaloongozwa na wataalamu waliobobea katika nyanja za kuimarisha uchumi katika ngazi ya Jamii , Local Economic Development. Mada zitakazojadiliwa ni pamoja na maana halisi ya dhana ya ukuzaji uchumi katika jamii umuhimu wa  taasisi za kifedha  katika kusaidia uendelezaji uchumi katika Jamii pamoja na  mada ya fursa zilizopo katika Halmashauri za  mijini na zile za wilaya katika ukusanyaji wa rasilimali (fedha).
Viongozi wa Serikali wamealikwa kutengeneza jopo la wasemaji. Miongoni mwa wanaotarajiwa ni Mhe. Stephen Wassira – Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Uhusiano, Mhe. Sospeter Muhongo (mb) Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (Mb) Waziri wa Maji Mhe. Hawa Abdur Rahman Ghasia (Mb) Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Gaudensia Kabaka (mb) Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Emanuel Nchimbi (mb) Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.  Profesa Ana Tibaijuka (mb) Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (mb) Waziri wa Maliasili na Utalii. Wengine ni Waziri wa Afya Dr Hussein Mwinyi (mb), Mhe. Dr John Pombe Magufuli (mb) – Waziri wa Ujenzi, Mhe. Mary Nagu (mb) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji na Mhe.  Makongoro Mahanga (mb) Naibu Waziri Kazi na Ajira. Waalikwa wengine ni pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Bwana Hari Kitilya, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Huduma za Manunuzi Dr. Ramadhani Mlinga pamoja na Mwakilishi wa Benki ya Dunia. Jumuiya imemwalika Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Fedha za Serikali (CAG) Ndugu Ludovick Utouh ambaye atawasilisha Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Fedha za Serikali za Mitaa.
Maandalizi ya Mkutano yamekamilika na ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru wabia na wadhamini walioweza kujitokeza kutuunga mkono katika Mkutano huu; NMB ambaye ni mdhamini mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), TASAF, na PSPF. Wengine ni PPF, Mamlaka ya viwanja vya ndege, Tanzania Standard Newspaper na GF trucks.
________________________________________
Dr. Didas  Massaburi – Mwenyekiti ALAT (T)
na Mstahiki Meya wa Jiji  la Dar es Salaam.     Leo Jumatano, tarehe 8 Mei 2013.

29TH ALAT AGM


Friday, April 27, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 24th Mei,2012
MKUTANO MKUU WA 28 WA ALAT - JUKWAA LA USHIRIKISHWAJI WA SEKTA BINAFSI
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itakua na Mkutano Mkuu wa 28 tarehe 3 – 5 Mei 2012. Mkutano huo utafanyika hapa Dar es Salaam kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.



Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa 28 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni “Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi”. ALAT imedhamiria kutumia Mkutano wake Mkuu wa Jumuiya kwa mwaka huu kuwa jukwaa la kupeana uzoefu wa ushirikiano baina ya sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP). Hii inatokana na sheria ya ubia iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania The Public Private Partnership (PPP Act) 2010. Mkutano huo ambao utafanyika tarehe 04- 05 Mei 2012, utatanguliwa na jukwaa la ubadilishanaji uzoefu juu ya ubia baina ya Serikali na sekta binafsi katika kutoa huduma kwa jamii na hasa katika kuzitumia Serikali za Mitaa. Ifahamike ya kwamba Serikali za mitaa sawa na majukumu yake, ndio zenye fursa ‘potential’ kubwa  na  nyingi za kutekeleza ubia kwa kufanya mashirikiano yenye manufaa na sekta binafsi. Jumuiya imeona haja na umuhimu wa kuandaa jukwaa hili kwa wanachama wake kwani ni lenye manufaa makubwa ya kuwafanya viongozi na watendaji wa Halmashauri zote nchini kuweza  kujifunza na kufahamu dhana nzima lakini pia utendekaji halisi (Practicality) wa ubia. Hii pia ni fursa ya pekee kwa sekta binafsi, taasisi za Serikali na mashirika ya Umma kuweza kushiriki pamoja na viongozi na watendaji wa Serikali za Mitaa kujadili jambo lenye manufaa kwa pande zote. Aidha Jumuiya inatoa nafasi chache za udhamini wa Mkutano Mkuu ambao pia utatoa fursa ya kushiriki moja kwa moja katika jukwaa hilo.
Jukwaa la ubadilishanaji uzoefu litakaloongozwa na mtaalamu aliyebobea wa kimataifa katika nyanja za ubia baina ya sekta ya umma na binafsi (PPP), litajadili mada mbalimbali zinazohusu ubia. Mada hizo ni pamoja na maana halisi ya ubia, je ni ubinafsishaji?; njia mbalimbali za kufanya ubia; msingi wa kisheria wa ubia, uzoefu wa halihalisi ya ubia kimataifa; dhati/dhamira hasa ya ubia;  faida zinazoweza kupatikana kutokana na ubia; Mchakato wa ufanyikaji wa ubia na Uchaguaji wa miradi na upembuzi yakinifu. Mada nyingine ni Utambuzi wa viashiria vya hatari (risks) uchambuzi wake na upunguzaji; fursa za kifedha katika ubia; njia muafaka katika manunuzi; usimamizi wa ubia, uangalizi na tathmini.  
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe wake ni kama ifuatavyo: Wenyeviti na Mameya 133 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya, Wakurugenzi 133 wa Halmashauri, Wabunge 21 mmoja toka kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na Wizara, Idara za Serikali Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa, wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau wangine wa sekta ya Serikali za Mitaa. Aidha Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika na Makampuni na Wawakilishi wa Sekta Binafsi.  Inatarajiwa kwamba Mkutano huu utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (500).
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri zote za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna Halmashauri 133 zinazounganishwa na chombo hiki.
Dira ya Jumuiya ni kuwa na Serikali za Mitaa zinazojitegemea na zenye ufanisi katika kutoa huduma zinazokidhi viwango kulingana na vipaumbele vya wananchi wake.
Mwelekeo wa Jumuiya ni kutambulika kama chombo na sauti ya pamoja ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ikitoa huduma za kitaalamu na kiufundi kwa wanachama wake.
Katika mkutano huo Jumuiya imemwalika Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mgeni rasmi
Aidha watu mashuhuri wakiwemo viongozi wa Serikali na Sekta binafsi wamealikwa kutengeneza jopo la wasemaji. Miongoni mwa wanaotarajiwa ni Mhe. Mustafa Mkulo Waziri wa Fedha, Mhe. William Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. kapteni Mstaafu George Mkuchika Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Gaudensia Kabaka Waziri wa Kazi na Ajira, Mhe. Emanuel Nchimbi Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Mhe.  Profesa Ana Tibaijuka Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mhe. Ezekiel Maige Waziri wa Maliasili na Utalii. Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dr.Cyiril Chami, Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Shamsi Nahodha, Waziri wa Kilimo na Ushirika Mhe. Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Mifugo Dr. Mathayo David Mathayo. Walioalikwa wengine ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini Bwana Hari Kitilya, Inspekta Jenerali wa  Polisi Ndugu Saidi Mwema Bi Esther Mkwizu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Huduma za Manunuzi Dr. Ramadhani Mlinga pamoja na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Kwa namna ya pekee na kwa kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais, Jumuiya imemwalika Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Fedha za Serikali (CAG) Ndugu Ludovick Utouh ambaye atawasilisha Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Fedha za Serikali za Mitaa.